Tuesday, 21 June 2016

UKAWA WAENDELEA KUSUSIA BUNGE, LEO WATOKA BILA MBWEMBWE


Wabunge wa Ukawa wameendelea kususia vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson, lakini tofauti na jana, leo wametoka kimyakimya bila mbwembwe kama zozote.

Wabuge hao walitoka nje wakati kamati ya uongozi ya umoja huo imeingia kufanya kikao kujadili mustakabali wao.

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema watatoa taarifa kamili baada ya kumaliza kikao hicho.

Huu umekuwa mwendelezo wa wabunge hao wa upinzani kususia vikao vya bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika Dkt. Tulia huku kikao cha leo kikiwa ni kikao cha 17 mfululizo kwa wabunge hao kususa.


Jana wabunge hao waliziba midomo yao kwa karatasi nyeupe zilizoandikwa jumbe mbalimbali ikiwa kama njia mojawapo ya kuwasilisha matwaka yao ya kutomkubali Naibu Spika, Dkt. Tulia kwa madai ya kuwa hawatendei haki wabunge hao wa upinzani hasa kuhusu miongozo mbalimbali ndani ya Bunge.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment