Tuesday, 21 June 2016

TRUMP AKABILIWA NA HALI NGUMU KIFEDHA


Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican Donald J. Trump anaingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu akiwa na hali mbaya ya kifedha ambayo haijawahi kutokea katika historia ya wanaowania Urais wa Marekani kw akupitia vyama vikubwa.

Taarifa kutoka Tume ya uchaguzi ya Marekani iliyotolewa jana jioni inasema kwamba Trump aliuanza mwezi Juni akiwa na dola za Kimarekani milioni 1.3 mkononi, kiasi hiki ni sawa na mtu anayewania kiti cha ubunge Marekani.

Hali hiyo imeelezwa kuwa inamweka yeye na chama chake katika wakati mgumu zaidi.

Imeelezwa kuwa wakati Trump ana fedha hizo Hillary Clinton ameanza Juni na dola za Marekani milioni 42 kwa mujibu wa taarifa zilizorekodiwa na tume hiyo ya uchaguzi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment