Friday, 24 June 2016

Shelisheli kuwavaa Serengeti Boys

Serengeti boys
Timu ya soka ya Vijana ya Shelisheli, inatarajiwa kuwasili usiku huu kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu ya Serengeti Boys. Mchezo wa timu hizi mbili utachezwa Juni 26, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu hiyo inaingia wachezaji na pamoja na viongozi 25, waamuzi wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo huo Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, huko Shelisheli.
Mchezo huo ni wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 michuano itayofanyika nchini Madagasca.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment