Sunday, 12 June 2016

RUNGWE ASEMA BAJETI IJAYO HAITABADILI MAISHA YA WATANZANIA


Wakili na Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Hashim Rungwe amesema kuwa bajeti iliyopitishwa na serikali haitaweza kubadilisha maisha ya watanzania endapo serikali haitaweka nia ya dhati ya kubana matumizi yake.

Amesema kuwa matumizi makubwa ya serikali yanawabebesha mizigo mikubwa wananchi wa kawaida na matumizi hayo yanaonekana zaidi kwenye uwepo wa wafanyakazi wengi serikalini ambao hawana tija kwa taifa na majukumu yao yangeweza kufanywa na watendaji wengine hali inayoongeza gharama kubwa za kulipa mishahara.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment