Thursday, 2 June 2016

Polisi Dar wakamata wahamiaji 71

 
WAHAMIAJI 71 wamekamatwa na Jeshi la Polisi nchini wakiwa katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam wakiwa ndani ya lori wakiingia nchini kwa njia haramu.
Kwa mujibu wa Ofisa Uhamiaji Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, George Gule wahamiaji hao haramu walikamatwa juzi usiku na jana walipewa taarifa na Polisi na kwenda kuwachukua katika eneo la ufukwe walipokamatwa na Polisi wakiwa ndani ya lori hilo.

Alisema lori hilo lilikamatwa na wahamiaji hao haramu pamoja na Watanzania wawili ni dereva na utingo wa lori hilo, ingawa inadaiwa kuwa aliyekuwa wakala wa wahamiaji hao haramu alikimbia.
Kwa mujibu wa utingo, Abraham Kapara, dereva wake alimueleza kuwa wanaenda kuchukua mzigo wa maboksi katika eneo hilo, lakini wakakuta ni watu hao. Lori hilo lilileta ndizi jijini Dar es Salaam kutoka mkoani Mbeya. Wahamiaji hao haramu wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment