Sunday, 12 June 2016

OLE MEDEYE WA CHADEMA ATIMKIA UDP


Mwanasiasa mashuhuri na kada wa Chadema na mbunge wa zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye ametangaza kukihama rasmi chama chake cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) na kujiunga na    chama cha UDP.


Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa Habari jijini Dar es salaam katika ofisi za Makao Makuu ya chama cha UDP Mwananyamala  leo, Ole Medeye amesema amechukua uamuzi huo kutokana na  kile alichosema kuwa wabunge wa Upinzani hawamuheshimu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Tulia Akson.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment