Wednesday, 15 June 2016

MKE WA MUUAJI WA MASHOGA KUFIKISHWA MAHAKAMANI


Mke wa Omar Mateen ambaye alihusika na mauaji ya watu 49 katiia klabu ya usiku ya mashoga mjini Orlando huenda akafunguliwa kesi inayohusiana na mauaji hayo.

Waendesha mashitaka wamekutaka mjini hapa kumchunguza Noor Salman.
Imeelezwa kuwa aliwaambia Polisi kwamba alijaribu kumshawishi mumewe asishambulie klabu hiyo ya  Pulse.

Tkatika shambulio hilo ambalo limeelezwa kuwa kubnwa katika historia ya uhalifu wa aina hiyo watu 53 walijeruhiwa wengine vibaya na mateen kuuawa na askari maalumu wa kukabili ugaidi.

Waendesha mashtaka wamesema kwamba watamshtaki mke huyo kw amakosa 49 ya mauaji,53 kujaribu kuua na kushindwa kwake kuitaarifu mamlaka juu yab uwezekano wa shambulio hilo kufanywa.

Mwendesha mashataka wanasema kwamba wanamchunguza kwa kuwa huenda mke huyo alipigiwa simu wakati Mateen anatekeleza kazi yake ya mauaji.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya ujasusi ya seneti ya Marekani, Seneta Angus King, ambaow alipewa taarifa za hali halisi alisema kwamba  inaonekana mwanamke huyo alikuwa anajua  mambo yalivyokuwa yakiendelea.

Wakati huo huo Rais Barack Obama amekerwa na  kauli ya mgombea Urais wa Marekani kw atiketi ya Republican ya kupiga marufuku waislamu kutokana na tukio hilo la Orlando.

Rais huyo alisema kwamba tamko la Trump si  lka namna ambavyo Marekani inastahili kuwa na kujengwa.


Alisema kuwatofautisha waislamu kulata zogo zaidi na kuifanya Marekani kutokuwa salama.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment