Thursday, 2 June 2016

MISS IRINGA KUPATIKANA KESHO MBELE YA WEMA SEPETU NA TIMU YAKE
MSANII nguli wa  wa filamu nchini na miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kesho anatarajia kushiriki fainali ya  shindano la kumsaka mlibwende atakaye uwakilisha mkoa wa Iringa katika shindano la Miss Tanzania 2016.

Shindano hilo lenye jumla ya washiriki 10 linatafanyika kesho Ijumaa, Juni 3 katika ukumbi wa Kichangani, mjini Iringa huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela .

Muandaaji shindano hilo, Maya Said alisema kuwa maaandalizi ya fainali hiyo tayari yamekishwakamilika kwa kiasi kikubwa na kuahidi kwamba “kwa jinsi warembo wazuri walivyojitokeza kushiriki nina hakika, Miss Tanzania  2016 atatoka mkoani Iringa kwa mara ya kwanza katika hostoria ya mashindano hayo.”

Alisema shindano hilo linakwenda sambamba na lengo lake la kuutangnaza mkoa wa Iringa kwa kuzingatia kauli mbiu yake ya Usafi wa Mazingira na Utalii wa Ndani.

Alisema kwa kuzingatia ubora wa washiriki wa shindano hilo mwaka huu, watatumia majaji wenye uzoefu na uwezo mkubwa akiwemo mmoja toka nchini Kenya.

Maya alisema kuwa mbali na Wema Sepetu kutakuwepo na wasanii  wa bongo fleva watakaombatana na timu ya kampuni ya Endless Fame akiwepo Mirror aka Kioo na Jordan pamoja na wasanii lukuki wa mkoa wa Iringa.

Mmoja wa washiriki hao Laula Kwai alisema kuwa wamefanya mazoezi ya kutosha na wanauhakika Miss Tanzania 2016 atatoka mkoani Iringa kwa kuwa wako vizuri na wanakidhi vigezo vya kuliwakilisha Taifa.

Kwa upande wake mmoja wa kamati ya maandalizi ya miss Iringa Viviani Kimati alisema walitumia vigezo vinavyotakiwa kuwapata warembo hao ambo wengi wao ni wanafunzi wa vyuo vikuu vya mjini Iringa.

Aliwataka wajiamini na wasifikirie rushwa ya ngono ili washinde katika shindano hilo, kanda na taifa na badala yake wazingatie mafundisho waliyopewa na  walimu wao walipokuwa  katika kambi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment