Monday, 27 June 2016

Messi ajiuzulu baada ya kukosa penalti

Mshambulizi wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amestaafu kutoka soka ya kimataifa.
Mchezaji huyo bora zaidi duniani alitangaza hatua hiyo baada ya kukosa penalti iliyoiwezesha Chile kuilaza Argentina katika fainali ya mchuano wa Copa America.
"Kwangu mimi ,soka ya kimataifa ama hata kuichezea Argentina sitaweza tena.
''Nimefanya kila niwezalo.''
''Kwa kweli inaniumiza kuwa sijawahi kutwaa kombe lolote la kimataifa'' alisema mshambulizi huyo mwenye umri wa mia 29.
Mshambulizi huyo ameisaidia mabingwa wa ligi kuu ya Uhispania Barcelona, kutwaa mataji 8 na mataji manne ya ubingwa wa bara ulaya.
Hata hivyo kimataifa Messi amewahi kushinda taji moja tu lile la nishani ya dhahabu ya Olimipiki ya mwaka wa 2008 Olympic.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment