Friday, 10 June 2016

Kumekucha Euro 2016

WENYEJI Ufaransa leo wanatarajia kufungua pazia la michuano ya Euro 2016 dhidi ya Romania huko Stade de France, huku kikosi cha Didier Deschamps kikipewa nafasi kubwa ya kushinda taji. Mabingwa mara mbili Ufaransa wanatabiriwa kulingana na Ujerumani na Hispania kwa kushinda mataji matatu ya Ulaya.
Les Bleus inajipanga kuwa taifa la kwanza mwenyeji kushinda taji tangu ilipofanya hivyo mwaka 1984, lakini katika michuano ya karibuni ilishuhudia ikishindwa zaidi ya robo fainali tangu ilipotwaa taji kwa mara ya mwisho mwaka 2000.
Ufaransa inaingia kwenye michuano hiyo ikiwa na kiwango kizuri baada ya kushinda mechi tisa katika mechi 10 za mwisho katika maandalizi yao ikiwa ni pamoja na ile iliyoshinda mabao 3-0 dhidi ya Scotland mwishoni mwa wiki iliyopita.
Deschamps alishambuliwa kwenye uteuzi wake wa timu baada ya mshambuliaji nyota Karim Benzema kuachwa kikosini kutokana na kuwa kwenye tuhuma za kumpiga picha za ngono mchezaji mwenziwe wa timu ya taifa, Mathieu Valbuena.
Antoine Griezmann anatarajiwa kuziba nafasi moja kati ya tatu za ushambuliaji akiwemo pia Kingsley Coman, Andre-Pierre Gignac, Olivier Giroud, Anthony Martial na Dimitri Payet wakipigania nafasi nyingine mbili.
Giroud amekuwa na mapokezi tofauti na mashabiki wa Ufaransa licha ya kufunga mabao saba katika mechi zake tano za mwisho alizoanza, wakati Payet alifunga mabao matatu kuipa timu ushindi dhidi ya Cameroon Mei 30, kiwango ambacho pengine huenda kikampa namba.
“Griezmann ana furaha,” alisema Deschamps alipozungumza na L’Equipe kuhusu mechi hiyo na kuongeza kuwa: “Amekuwa na msimu mzuri Atletico na kipaumbele chetu cha kwanza ilikuwa kumpatia muda wa kupumzika kwanza kabla ya kuanza kwaa michuano.”
“Antoine ana kiwango kinachomfanya kuwa miongoni mwa washambuliaji bora Ulaya, mara zote amekuwa mchezaji mzuri, lakini mara zote amekuwa imara pia.” Baada ya kuumia kwa Lassana Diarra, mchezaji wa Leicester City N’Golo Kante anatarajiwa kuziba pengo la kuwa kiungo wa mwisho pamoja na Blaise Matuidi na Paul Pogba, huku Adil Rami akionekana kuzishinda mbio za kuwania namba ya beki wa kati na Laurent Koscielny nafasi yenye mabeki wazuri akiwemo Raphael Varane ambaye ni majeruhi.
Les Bleus haijafungwa katika mechi 10 dhidi ya Romania, lakini mechi nne kati ya tano za mwisho walizokutana zilimalizika kwa sare huku kikosi cha Anghel Iordanescu kikiwa na safu nzuri ya ulinzi katika mechi za kufuzu, kimefungwa mabao mawili tu katika mechi 10.
Mataifa hayo mawili yalikutana mara mbili kabla ya hatua ya makundi ya michuano hiyo, mechi ya kwanza Ufaransa ilishinda bao 1-0 mwaka 1996 na ya pili zilitoka sare ya bila kufungana kwenye Euro 2008. Romania haina wachezaji wengi wazoefu wa michuano ya kimataifa katika kikosi chake, kina wachezaji wengi wenye umri wa miaka 23 ambao wamecheza mechi 22.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment