Tuesday, 14 June 2016

Je,wajua kunenepa sana huchangia utapia mlo?

Kunenepa kupitia kiasi
Utafiti mpya unaonyesha visa vinavyoongezeka vya watu kunenepa kupitia kiasi huchangia kukuwa kwa tatizo la utapia mlo.
Kawaida utapia mlo umehusishwa na upungufu mkubwa wa chakula lakini utafiti huu umedhihirisha kuwa ulaji wa vyakula visivyo bora kwa afya, husababisha ulimbikizaji wa sukari, chumvi na mafuta ya cholesterol huku mwili ukipungukiwa na madini muhimu yanayohitajika ili kujenga siha na afya njema.
Ripoti hiyo inaonya kuwa iwapo hatua mwafaka hazitachukuliwa kukabiliana na tatizo la uzito kupindukia litapelekea kudorora kwa viwango vya hali ya afya duniani.
Utapia mlo umekuwa ukihusishwa na watoto ambao hawana chakula hawakui na kwamba wanakabliwa na maambukizi.
Haya bado ni maswala makuu,lakini kuna maendeleo yalioafikiwa katika sekta hiyo.
Ripoti hiyo inatoa changamoto zinazosababishwa na kunenepa kupitia kiasi.
Kunenepa sana
Ongezeko la watu wanene kupitia kiasi limeanza kuonekana katika kila eneo la ulimwengu katika kila nchi.
Mamia ya mamilioni ya watu huugua utapia mlo kwa sababu ya kuwa na sukari nyingi,chumvi na mafuta katika miili yao,ripoti hiyo imesema.

Source: http://www.bbc.com/swahili/

Reactions:

0 comments:

Post a Comment