Saturday, 11 June 2016

Ibada ya kumkumbuka Ali yajawa na mihemko

Baadhi ya mabondia na muigizaji Will Smith waliohudhuria hafla hiyo. Umati watu 14000 ulisikiliza kwa makini watu wa tabaka na dini tofauti wakimuomboleza mohammed ali kutokana na umahiri wake katika ulingo wa michezo na pia alivyoitunza jamii, huku wakisifu mchango wake katika kuimarisha amani duniani na haki za binadam.
Umati wa watu waliohudhuria hafla ya kumbukumbu hiyo
 Mkewe Ali, Lonnie Ali, anasema mumewe alikabiliwa na masaibu si haba, bila kuonyesha hasira, na kuwataka watu kufuata mfano wake.
Mkewe Muhammad Ali


Msafara wa mwili wa Muhammad Ali kabla ya kuzikwa nyumbani Louisvile Kentucky siku ya Ijumaa
Katika taarifa, rais wa Marekani Barrack Obama, alimtaja Ali kama mtu shupavu, aliyeng'aa na aliyekuwa na ushawishi mkubwa kuliko mtu yeyote wa kizazi chake.

 Rais wa zamani Bill Clinton, alikumbuka utanashati, ucheshi na utu aliooonyesha marehemu Ali, wakati akikabiliana na machungu ya ugonjwa uliomdhoofisha.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment