Tuesday, 21 June 2016

DK MWAKYEMBE AKANUSHA UTAPELI WA SH BILIONI 2


Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe amesema kuwa atalishtaki mahakamani gazeti la Dira ya Mtanzania kwa kuandika habari inayomhusisha na utapeli wa shilingi bilioni 2.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwakyembe ambaye amekanusha vikali habari hizo zilizoandikwa na Dira ya Mtanzania toleo la Juni 13 mwaka huu, amesema kuwa gazeti hilo limeonesha dhahiri kuwa limekosa weledi na limepotosha kwa kiasi kikubwa.

“Nakiri kuwa sijawahi kushuhudia upotoshaji mkubwa wa makusudi kama huu. Ukiisoma taarifa ya gazeti hili utaona waziwazi umakini na weledi wa habari unakosekana, hata jina la wizara yangu limekosewa,” alisema Mwakyembe.

Mwakyembe alisema tayari mawakili wake wameanza mchakato wa kufungua kesi mahakamani ili kulishitaki gazeti hilo kwa upotoshaji.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment