Tuesday, 17 May 2016

Yanga yaongezewa fedha ubingwa Ligi Kuu


Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas
ZAWADI za bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara imeongezeka, ambapo Yanga watapewa kitita cha Sh milioni 81.3 badala ya Sh milioni 80 ilizozawadiwa msimu uliopita.
Yanga imetwaa nafasi ya kwanza, ambapo hadi sasa imejikusanyia jumla ya pointi 72 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine 15 zinazoshiriki ligi hiyo, inayofikia kilele Jumapili.
Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema jana kuwa, wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi Vodacom, watatoa Sh 81,345,723 kwa mshindi wa kwanza.
Lucas alisema mshindi wa pili, nafasi inayogombewa na Azam na Simba ataondoka na Sh 40,672,861 wakati mshindi wa tatu atapewa Sh 29,052,044 na wa nne ataondoka na Sh 23,241,635.
Alisema kuwa mchezaji bora, mfungaji bora na kipa bora kila mmoja ataondoka na kitita cha Sh 5,742,940 huku mwamuzi bora na kocha bora kila mmoja ataondoka na Sh 8,614,610 wakati timu yenye nidhami itapata Sh milioni 17.
Msimu uliopita mshindi wa pili ambaye ni Azam FC aliondoka na Sh milioni 40 wakati Simba iliyotwaa nafasi ya tatu ilipewa Sh milioni 28 na Mbeya City iliyomaliza ya nne ilibeba Sh milioni 22.
Mfungaji bora msimu uliopita alikuwa Simon Msuva wa Yanga ndiye alitwaa Sh milioni 5.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment