Tuesday, 17 May 2016

WHO: Madaktari wasiwakekete wanawake


Shirika la afya duniani ;imewaonya madaktari wasijihusishe na ukeketaji
Mwongozo mpya wa shirika la afya duniani umewaonya madaktari wasijihusishe katika kille kilichotajwa kama "matibabu"wa ukeketaji wa wanawake.
Katika kushughulikia suala hilo shirika hilo limesema kuwa wazazi wakati mwingine wananaweza ''kumuomba muhudumu wa afya kufanya ukeketaji kwasababu wanafikiri itappunguza madhara ya ukeketaji ".
Daktari wa shirika hilo (WHO) Dr. Lale anasema : " Ni tatizo kwamba wahudumu wa afya wenyewe wanaendeleza vitendo hivi hatari bila kupenda ."
Muongozo huo mpya ambao pia unahusu tiba za magonjwa ya ngono na ya akili, umetolewa kwasababu ''wahudumu wa afya mara kwa mara hawafahamu madhara ya kiafya ya ukeketaji na wengi hawana mafunzo ya kutosha ya kutambu na kutibu madhara hayo ipasavyo ".

Reactions:

0 comments:

Post a Comment