Wednesday, 18 May 2016

WAREMBO 15 KUTOANA JASHO MISS MBEYA 2016
WAREMBO 15 wanatarajia kufuana kuwania taji la Miss Mbeya 2016, litakalofanyika katika ya hotel ya Paradise iliyopo Sowetho  Jijini Mbeya.

Walimbwende hao wanaowania taji hilo linaloshikiliwa na Irene Luvanda kuwa ni pamoja na Emmaniliana Abdala, Anitha Patric, Aziza Lyasamuya, Praxeda Geofrey, Juliana Gilbert Nancy Matta, Agnes Baliva, Julitha Mponela, Afrodisia Chapa, Eunice Robert, Priscar Mengi na Julina Lyampawe. 

Shindano hilo la ulimbwende lenye mvuto mkubwa nchini litakalofanyika Mei 20 katika ukumbi wa hoteli hiyo, litasindikizwa na burudani kapambe kutoka kwa msanii wa kizazi kipya, Homonize  a.k.a Simba mtoto. 

Mratibu wa Shindano hilo Tom Chilala ambaye pia ni Meneja wa Radio ya Dream FM amesema warembo hao watapanda jukwaani na kuonesha umahiri wao katika utembeaji wa madaawakiwa katika mavazi tofauti, yakiwemo ya ubunifu, ufukweni na yanayovaliwa jioni.

Alisema shindano hilo linatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa fani ya urembo na sanaa rembo kutoka Jiji la Mbeya na Viunga vyake ambao wanashahuku kutokana na kuwaanda vyema warembo hao. 

Chilala alitaja zawadi kwa mshindi wa kwanza kuwa ni fedha tasilimu Sh 700,000,wa pili Sh 400,000, wa tatu Sh 200,000 na washiriki wengine wataambulia Sh 80,000 kwa kila mmoja kama kifuta jasho zitakazokabidhiwa kwa warembo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla anayetarajiwa kuwa mgeni wake rasmi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment