Tuesday, 24 May 2016

VIWANDA VIPYA VYA KUSINDIKA MAZAO YA KILIMO VYAJENGWA UKANDA WA SAGCOT


UKANDA wa Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) umeanza kupata mafanikio baada ya wawekezaji kuanza kujenga viwanda vya kusindika mazao vitakavyoongeza ajira na soko la mazao ya wakulima hasa wadogo.

Viwanda vitatu vipya vya kusindika nyanya na mazao ya mifugo vimejengwa katika mkoa ya Iringa ulioko katika kongani ya Ihemi inayojumuisha mikoa ya Iringa na Njombe kupitia program hiyo ya SAGCOT (Viwanda viwili) na Morogoro uliopo katika kongani ya Kilombero (kiwanda kimoja).

Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga alisema hayo hivikaribuni mjini Njombe katika kikao cha mapitio ya utekelezaji wa programu ya SAGCOT katika kongani ya Ihemi kilichohusisha wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya za mikoa ya Iringa na Njombe.

Kirenga alisema wakati Iringa Mjini kimejengwa kiwanda kipya chenye uwezo wa kusindika tani 200 za nyanya kwa siku na cha kusindika vyakula vya mifugo kwa kutumia mahindi, soya na mashudu ya alizeti chenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 130 kwa siku, mkoani Morogoro kinajengwa kiwanda cha kusindika mazao ya mifugo hasa kuku na samaki.

Alisema kukamilika kwa viwanda hivyo mjini Iringa kumewaongezea soko wakulima wa Iringa, Njombe, Ruvuma na Mbeya wanaoweza kuvitumia kuuza zaidi ya tani 300 za mazao yao kwa siku. Tunahitaji viwanda vingine zaidi ya hivyo Moro kuna kiwanda vya kusindika mazao ya mifugo hasa kuku na samaki.

Kirenga alisema katima mikoa hiyo yenye eneo linalozalisha asilimia 65 ya chakula kinachozalishwa nchini, mazao ya biashara na chakula kama mahindi, kahawa, mpunga na chai, sehemu yake kubwa yanauzwa yakiwa ghafi kwasababu ya ukosefu wa viwanda.

Alisema eneo hilo ni moja kati ya maeneo bora ya kilimo Afrika na ndio sababu serikali na wabia wa kilimo wamekubaliana kutoa kipaumbele katika ukanda huo kabla ya kuendelea na maeneo mengine nchini.

“Kwa kuzingatia sera ya Rais Dk John Magufuli, nchi hii imeanza safari ya uchumi wa viwanda ambayo sehemu kubwa itajengwa kutokana na kazi inayofanyika katika eneo hilo la kilimo la SAGCOT kwahiyo tunahitaji viwanda vingi zaidi vya kusindika mazao ili kuongeza thamani ya kile kinachozalishwa shambani,” alisema.

Kirenga alisema katima mikoa hiyo yenye eneo linalozalisha asilimia 65 ya chakula kinachozalishwa nchini, mazao ya biashara na chakula kama mahindi, kahawa, mpunga na chai, sehemu yake kubwa yanauzwa yakiwa ghafi kwasababu ya ukosefu wa viwanda.

Alisema programu ya SAGCOT inayohusisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Iringa, Rukwa, Mbeya, Ruvuma, Njombe na Katavi iliyogawanywa katika kongani sita za Ihemi, Rufiji, Kilombero, Mbarali, Ludewa na Sumbawanga ilianza kutekelezwa mwaka 2011.

“Programu itakwenda hadi mwaka 2030, lengo likiwa ni kuwekeza zaidi ya Dola za Marekeni Bilioni 3.5 katika ukanda huo na kati yake Dola Bilioni 2.4 zitokane na uwekezaji wa sekta binafsi na zinazobaki zitawekezwa na sekta ya umma katika miundombinu, mawasiliano na huduma za jamii,” alisema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment