Sunday, 22 May 2016

VAN GAAL KUONDOKA MAN U?


Kuna uwezekano mkubwa sana ndani ya wiki hii uongozi wa Man United uliyokuwa umekaa kimya kwa muda mrefu, ukatoa taarifa rasmi kuhusu hatma ya kocha wao Louis van Gaal, kwani kuna dalili kubwa kocha huyo akaondoka kutokana na kauli yake aliyoitoa wakati akitoka katika hoteli ya timu.

Louis van Gaal ambaye alikuwa akitoka katika hoteli ya timu alimwambia ripota wa Sky Sport News “It’s over” kauli ambayo imetafsirika kuwa huo ndio mwisho wake ndani ya klabu ya Man United, hivyo watu watarajie chochote kinaweza kutangazwa na uongozi wa Man United kuanzia hivi sasa.


Mitandao na vituo vikubwa vya Tv barani  Ulaya hususani Uingereza, jana May 21 2016 walitangaza habari kuwa klabu ya Man United imemchagua kocha wa zamani waChelsea Jose Mourinho kurithi nafasi ya Louis van Gaal ambaye muda wowote kuanzia hivi sasa atatangazwa kuachishwa kazi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment