Sunday, 8 May 2016

TRA LINDI YATAIFISHA SUKARI NA KUGAWA BURE KWA WANANCHI


Mamlaka ya Mapato (TRA), Mkoa wa Lindi imetaifisha na kugawa sukari mifuko 5,319 kutoka nchini Brazil yenye thamani ya shilingi 373.5 milioni na kuigawa kwa taasisi mbalimbali kama ilivyoagizwa na Rais, Dkt. John Magufuli hivi karibuni.

Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari, mwaka huu wakati ikiwa inaingizwa nchini kimagendo kutoka nchini Brazil.

Taasisi za mkoa huo zilizogawiwa sukari hiyo ni pamoja na magereza, shule maalum, kambi za wazee, shule za kawaida na hospitali.

Hivi karibuni Rais Magufuli alitoa onyo kwa wafanyabiashara wanaoficha sukari ilhali kukiwa na uhaba mkubwa wa sukari kwa wananchi hali iliyopelekea bidhaa hiyo kupanda bei kwa kasi ya ajabu na kuwafanya wananchi wengi wa hali ya chini kushindwa kumudu bei hizo.


Rais Magufuli mbali na kutoa onyo hilo kwa wafanyabiashara hao, ameagiza sukari yoyote itakayopatikana imefichwa au kuendeshwa kimagendo itaifishwe na kugawiwa bure kwa wananchi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment