Tuesday, 10 May 2016

TANI 11,000 ZA SUKARI ZAWASILI NCHINI


Katika kukabiliana na uhaba wa sukari nchini, Serikali imesema tayari imekwishaingiza nchini tani 11,000 za sukari huku zingine zikitarajiwa baada ya muda mfupi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema sukari hiyo itagawiwa nchi nzima katika kanda za kaskazini,mashariki, kanda ya ziwa, nyanda za juu kusini na kati kwa uwiano utakaoendana na mahitaji husika.

Amesema kwa hapa nchini uzalishaji wa sukari utaanza rasmi mwezi wa saba mwaka huu ambapo zaidi ya tani 24,000 zinatarajiwa kuzalishwa.


“Sukari hiyo itasambazwa katika masoko na kuuzwa kwa bei ileile ya shilingi 1,800 iliyowekwa na serikali,” amesisitiza Waziri Mkuu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment