Friday, 20 May 2016

SERENGETI BOYS NUSU FAINALI INDIATIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ jana ilifuzu kwa hatua ya nusu fainali ya michuano maalumu ya kimataifa yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka India inayoendelea nchini humo kwa lengo la kuipa makali timu ya taifa ya nchi hiyo itakayokuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia kwa vijana mwaka kesho.
Imetinga hatua hiyo baada ya jana kutoka sare ya mabao 2-2 na Korea Kusini, mchezo uliofanyika Uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa. Katika mchezo huo, mabao ya Serengeti yalifungwa na Assad Juma katika dakika ya 12 na Maulid Lembe katika dakika ya 87 ambaye alisawazisha baada ya Korea kutangulia kwa mabao 2-1.
Matokeo hayo yanaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi tano na kwamba inasubiri matokeo ya mwisho kati ya Korea Kusini na Marekani yatakayotoa mwanga wa timu itakayocheza fainali.
Nyota wa Serengeti Boys kesho watacheza na Malaysia. Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25, 2016 na kabla ya mchezo wa fainali, utachezwa mchezo wa mshindi wa tatu katika uwanja huo huo wa Tilak Maidan.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment