Saturday, 7 May 2016

Nduguye Bush asema hatompigia kura Trump

Trump na Jeb Bush katika mjadala awa siku za nyuma
Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Jeb Bush, amesema kuwa hatampigia kura Donald Trump katika Uchaguzi wa Novemba.
Bwana Bush alisema kuwa Trump hana tabia wala mienendo ya kuwa Rais wa Marekani.
Jeb ni mojawapo wa wanachama mashuhuri wa Republican kutanganza hadharani kuwa hatompigia kura Bwana Trump kwa sababu ya kampeni yake ya kiburi ambayo imegawanya chama cha Republican.
Mnamo Alhamisi Spika wa Bunge, Paul Ryan, alisema kuwa hatamuunga mkono mfanyabiashara huyo tajiri, ingawa atakutana naye juma lijalo.
Hata hivyo Bwana Trump ameungwa mkono na mgombezi wa Urais wa zamani Bob Dole aliyeshindwa katika uchaguzi na Bill Clinton wa chama cha Democratic mwaka 1996.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment