Saturday, 7 May 2016

Marekebisho sheria ya ndoa bungeni SeptembaSERIKALI inatarajia kuwasilisha bungeni Septemba mwaka huu marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ili kuondoa vipengele vyote kandamizi kwa watoto.
Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangallah wakati wa majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2016/2017, baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Koshuma Kiteto (CCM) kuondoa shilingi akitaka Sheria ya Ndoa kurekebishwa ili mtoto asiolewe akiwa na miaka 14.
Hata hivyo baadaye alirejesha shilingi baada ya kuridhika na majibu ya naibu waziri huyo. Dk Kigwangallah alisema lengo la serikali ni kuwafanya watoto wa kike waweze kusoma na wasikumbane na ukandamizaji wa aina yoyote.
Naye Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe akitoa ufafanuzi wa sheria hiyo kutofanyiwa marekebisho kwa muda mrefu alisema wakati wa serikali ya awamu ya Nne walishindwa kufanyia marekebisho kutokana na unyeti wake kwa upande wa dini.
“Baraza la mawaziri likaamua tutoke na ‘white paper’, tuhoji wananchi wenyewe ndio waseme wanachotaka bila hivyo hata kesho serikali tunaweza kuleta marekebisho… lakini kutokana na suala la katiba mpya tukalisogeza suala hili.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment