Tuesday, 17 May 2016

Mamilioni waipongeza Leicester City


Mashabiki wa Leicester City
Watu wanaokadiriwa kuwa robo milioni wameandamana kwa lengo la kuipongeza klabu ya Leicester city iliyoibuka bingwa wa ligi kuu ya England baada ya miaka 132 ya historia yake.
Mistari miwili mikubwa pamoja na gari kubwa lililo wazi vilizunguka mji huo ulio katikati ya Uingereza.
Meneja wa Leicester Muitaliano Claudio Ranieri ameiambia BBC kuwa mji mzima ulifurika watu waliokuwa wakiishangilia timu yao ambayo ilicheza kwa kujitolea sana.Baadaye akapaza sauri kwa nguvu akiuambia umati uendelee kusherehekea:''endeleeni kuota,msiamke!
Leicester walipewa nafasi moja tu kati ya 5000 ya kushinda taji hilo la ligi mwanzoni mwa msimu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment