Tuesday, 19 April 2016

Watu 22 wauawa Afghanistan Kundi la Taliban ladai kuhusika


Rais wa Afghanistan Ashraf Ghan amethibitisha kuuawa kwa watu 22 na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia shambulizi la kujitoa mhanga lililotokea kwenye mji mkuu wa Afghanistan Kabul.
Mashuhuda wanasema kwamba watu kadha waliokuwa wamejihami, waliingia kwenye majengo yaliyo karibu na makao ya shirika la ujasusi la nchi hiyo na kufanya mashambulizi hayo.
Msemaji wa wizara ya ndani amesema kuwa eneo hilo kwa sasa limefungwa na vikosi vya usalama ambapo ulinzi kuimarishwa katika eneo hilo.
Aidha kundi la Taliban lilitangaza kutekeleza shambulizi hilo

Reactions:

0 comments:

Post a Comment