Wednesday, 27 April 2016

UKAWA KUKOMAA UDA IREJESHWE KWA WANANCHI


Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea amesema Halmashauri ya Jijiji la Dar es Salaam itahakikisha umiliki wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) unarudishwa kwa umma.

Amesema alichokisema CAG kuhusu UDA kimedhihirisha ambacho wamekuwa wakikisema kwa muda mrefu kuhusu mchakato mzima wa uuzwaji wa UDA kuwa ulikuwa wa rushwa, wizi, udanganyifu na matumizi mabaya ya madaraka.

“Sisi wabunge wa Dar es Salaam kupitia muungano wetu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) tumedhamiria kuirejesha umiliki wa UDA kwa umma kwa asilimia 100,” ameongeza.

Tunamuomba Rais, Dkt. John Magufuli atuunge mkono katika hili.
Tayari ripoti iliyotolewa mjini Dodoma na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Assad imeeleza kuwa hisa za UDA zilithaminishwa kwa bei ya Shilingi 744.79 kwa kila hisa Oktoba, 2009 na Novemba 2010 thamani ya kila hisa ikiwa Shilingi 656.15.

Kulingana na mkataba wa kuwasilisha hisa wa Februari 11, 2011, mnunuzi (kampuni ya Simon Group Limited) ilitakiwa kulipa Shilingi Bilioni 1.14 kwa bei ya ununuzi wa hisa zote.

Hata hivyo, mnunuzi alilipa Shilingi milioni 285 pekee katika akaunti namba OJ1021393700 ya benki ya CRDB inayomilikiwa na UDA.

Hatahivyo Mwenyekiti wa Bodi ya UDA, Idd Simba alipokea kiasi cha Shilingi milioni 320 kupitia akaunti yake binafsi kutoka kwa mwekezaji ambapo kwa mujibu wa Simba, ni ada ya ushauri alioutoa kwa mwekezaji jambo ambalo linaonesha kuwepo kwa mgongano wa masilahi.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment