Saturday, 16 April 2016

TAARIFA KWA UMMATAARIFA KWA UMMA

Uongozi wa Kampuni ya IVORI IRINGA (I. F. B) Unapenda kuutaarifu Umma Hususani Walaji, Wauzaji wa Jumla na Reja Reja kuwa 

kumekuwepo na bidhaa  ya CHOCOLATE ambayo inatoka NJE YA NCHI ambayo imefananishwa jina la Nembo ya Bidhaa zetu za IVORI CHOCOLATE na hivyo kuwachanganya wateja wetu juu ya uwepo wa bidhaa yetu hiyo nakujiuliza maswali yafuatayo

1-Je Tumebadilisha Jina la Kampuni yetu?
2-Je Tumebadilisha Muonekano wa Bidhaa yetu ya CHOCOLATE?
3-Je Tumebadilisha Bei ya Chocolate za Ivori?

Kutokana na maswali hayo yaliyojitokeza kwa Wateja wetu, Kampuni Ya IVORI IRINGA Inapenda kuutaarifu Umma yafuatayo

1-Kampuni ya IVORI-Iringa haijafanya mabadiliko yeyote juu ya muonekano wa bidhaa zake, Gharama yake  wala Nembo yake, haswa ya IVORI CHOCOLATE, Hivyo inawaomba wateja wake kuzingatia Yafuatayo

1-Kuhakikisha kila bidhaa unayonunua ya IVORI ina Nembo Halisi ya IVORI yenye Herufi I mwanzoni na herufi I  mwishoni.
isomeke IVORI CHOCOLATE na Sio IVORY CHOCOLATE

2-Bidhaa zetu zote zinatengenezwa TANZANIA,Tunajivunia Uzalendo wetu na ndio maana bidhaa zetu zote ni MADE IN TANZANIA .

3-Hakikisha kila  Chocolate yetu unayoinunua ina Rangi ya kahawia ndani ya pakiti yake ikiwa na Ladha tamu ya maziwa ikitegenezewa na COCOA Halisi inayolimwa na Wakulima Nchini TANZANIA

4-Rangi ya kifungashio chakeni ya Njano iliyochanganywa na Rangi ya Zambarau.

5-Gharama zetu Elekezi ni Shilingi 1000 kwa Gram 40 na Shilingi 500 kwa Gram 20 na hatuna ujazo unaozid gram 40.

KUWA MJANJA USIDANGANYIKE KUNUNUA BIDHAA FEKI,NUNUA BIDHAA ORIJINO ZA IVORI IRINGA,  EPUKA KUTAPELIWA.

ZINGATIA-Iwapo kuna utofauti wa Bidhaa unayoiona na kuitilia shaka Tafadhari usisite kuwasiliana nasi.
       Imetolewa na
MKURUGENZI MKUU
I. F. B

Reactions:

1 comments: