Wednesday, 27 April 2016

SERIKALI KUWASAKA WAFANYABIASHARA WANAOFICHA SUKARI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo amewaaagiza Maofisa  Biashara kuanzia ngazi ya  Wilaya, mikoa na Taifa kufanya ukaguzi wa wafanyabiashara wanaoficha sukari kwa maslai yao yanayolenga kuwawezesha kupata faida zaidi kwa kupandisha bei.

Akihitimisha mjadala wa hotuba ya Mapato na Matumizi ya ofisi yake, Waziri Mkuu amekiri kwamba kuna upungufu wa sukari nchini  unaochochewa na wafanyabiashara wanaofanya udanganyifu ili watengeneze faida.

Amesema takwimu zinaonesha kuwepo kwa tani 37,000 za sukari katika magahala mbalimbali nchini lakini haionekani katika soko.


Uchunguzi wa mtandao huu unaonesha bei ya sukari kwenye baadhi ya maduka katika mikoa mbalimbali nchini imepanda hadi kati ya Sh 2,300 na 2,500.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment