Tuesday, 19 April 2016

RAIS DR MAGUFULI ATUMBUA JIPU NI MKURUGENZI JIJI LA MAKONDA....


Dr Wilson Kabwe.
Rais John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Dr Wilson Kabwe.
Ametangaza uamuzi huo wakati akimalizia kuhutubia kwenye uzinduzi wa daraja la Kigamboni leo.
Kabwe amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuingia kwenye mikataba iliyosababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 3.

Akiwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Kabwe amehusika kwa kuiongezea kampuni ya utozaji ushuru wa parking jijini pamoja na ongezeko la kiwango cha faini halali ya shilingi 20,000/=hadi 80,000/=kwa kila kosa la wrong parking.

Akiongea na wananchi kwenye uzinduzi huo, Magufuli amesema wananchi wamelia kwa muda mrefu kutokana na ufisadi wa baadhi ya viongozi na kwamba zamu imefika kwa mafisadi kulia pia.

“Kwahiyo leo ni zamu ya Kabwe naye akalie kule na vyombo vianze kuchunguza hali halisi, wakimclear mimi sina tatizo, akikutwa kuna tatizo hatua zifuate, ndio maana hapa kazi tu.”

Reactions:

0 comments:

Post a Comment