Monday, 25 April 2016

POLISI JIJINI DAR ES SALAAM WAKAMATA OMBAOMBA 45


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema tayari limewakamata ombaomba 45, ambapo kati yao 17 wameshapelekwa gerezani.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Simon Sirro amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na ustawi wa jamii wanaaagalia utaratibu wa kuhakikisha watu hao wanarudishwa mikoani walipotoka badala ya kendelea kuwa ombaomba hapa mjini.

Akizungumzia zoezi zima la kuwaondoa ombaomba hao, Kamanda Sirro amesema kwa kiasi kikubwa zoezi hilo limeenda vizuri japo kuna baadhi ya ombaomba ambao bado wapo mitaani kwani hukimbia kila mara wanapowaona polisi.

Katika tukio lingine Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa 96 wenye umri wa kati ya miaka 15-18 wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya kuvamia na kupora nyakati za usiku katka maene mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment