Monday, 4 April 2016

MREMA ASALIMU AMRI KWA JAMES MBATIA


Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Vunjo kupitia TLP, Augustine Mrema amesalimu amri na kuamua kuitoa kesi ya uchaguzi aliyoifungua dhidi ya mbunge wa jimbo hilo James Mbatia (NCCR-Mageuzi) baada ya kukubaliana naye.

Jaji Lugano Mwandambo aliyekuwa akisilikiza shauri hilo aliamua kuifutilia mbali kesi hiyo baada ya Mzee Mrema kuamua kuitoa kesi hiyo mahakamani baada ya vuta nikuvute nyingi zilizomfanya Ndugu Mrema kukwama mara mbili baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Moshi kukataa kupokea vielelezo viwili muhimu kabla ya kuanza kutoa ushahidi wake .

Katika kesi hiyo, Mrema alikuwa anawalalamikia Mbunge wa Jimbo hilo, Mbatia (NCCR-Mageuzi), Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Vunjo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju huku akiiomba mahakama itengue ushindi wa Mbatia kwa madai kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.


Hata hivyo, kwenye uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana, Mbatia alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 60,187, akifuatiwa na Innocent Shirima (CCM), aliyepata kura 16,097 na Mrema kura 6,416.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment