Saturday, 9 April 2016

MREMA AMUANGUKIA MAGUFULI


Mwanasiasa mkongwe ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) taifa, Augustine Mrema amemuangukia Rais Dk John Magufuli ampe kazi ili amsaidie kutumbua majipu.

Mrema amemuomba Rais kazi wakati akiongea na Waandishi wa Habari kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro ambapo alisema kuwa wakati wa Kampeni Rais Magufuli alimuahidi kumpa kazi endapo angeshinda urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini cha kushangaza hadi sasa hajampa.

Alipoulizwa ni kazi gani inayomfaa katika Serikali ya Magufuli, alisema yeye alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu hivyo yuko tayari kufanya kazi yoyote itakayomfaa ila alitamani zaidi kupangwa sehemu nyeti ili amsaidie kutumbua majipu.


Mwanasiasa huyo pia  alikanusha taarifa ya kuhongwa fedha ili kufuta kesi ya kupinga matokeo aliyoifungua dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo, James Mbatia.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment