Monday, 4 April 2016

MDEE AMTAKA MAGUFULI ATAJE POSHO ANAZOLIPWA NJE YA MSHAHARA ALIOUTAJA


Mbunge wa Ukawa Halima Mdee ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) amemtaka Rais Magufuli kuweka wazi posho na marupurupu anayoyapata kama alivyoataja mshahara wake.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Sokoni, Jimbo la Mtama mkoani Lindi jana Mdee amesema wabunge wanalipwa mshahara wa Sh3 milioni, lakini kuna posho mbalimbali kutokana na kuhudumia wananchi ambayo inafika milioni 10, hivyo Rais anapaswa kutaja posho yake ili wananchi nao wajue.

Kauli hiyo ya Mdee imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kutaja mshahara wake kuwa ni Sh9.5 milioni kwa mwezi.

“Juzi Rais anasema eti mshahara wake Sh9.5 milioni, sasa atutajie posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi ambacho anakipata,” alisema Mdee.


Hivi karibuni wabunge wa Upinzani Tundu Lissu pamoja na Zitto Kabwe  waliibuka na kumtaka Rais Magufuli ataje Mshahara wake ambapo baada ya siku moja Rais Magufuli aliamua kutaja mshahara wake kupitia kituo cha Tv cha Clouds ya jijini Dar es salaam.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment