Thursday, 21 April 2016

Man United mabingwa wa soka ya chipukizi

Timu ya Vijana ya Manchester United miaka 21 kwa mwaka wa pili mfululizo imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya UIngereza baada ya kuifunga mabao 3-2 Tottenham jana Uwanja wa White Hart Lane.
Ushindi wao ulitokana na mabao yaliyofungwa na Andreas Pereira, Donald Love na Guillermo Varela.
Hilo ndilo taji la tatu kwa kikosi cha Warren Joyce ndani ya miaka minne.
Ushindi huo unawafanya United wafikishe pointi 45 katika msimamo wa Ligi Kuu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 England baada ya kucheza mechi 20, wakifuatiwa na Sunderland yenye pointi 43 za mechi 22.
Sunderland imemaliza mechi zake, wakati Man United ina viporo viwili dhidi ya Southampton na Chelsea.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment