Thursday, 14 April 2016

MAGUFULI KUZINDUA DARAJA LA KIGAMBONI NA UJENZI WA BARABARA ZA JUU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya TAZARA na ufunguzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mhandisi Joseph Nyamhanga   amesema  uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya juu utafanyika Jumamosi, Aprili 16, 2016  na Jumanne 19 Aprili 19, 2016, Mheshimiwa Rais atafungua rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5.

Ujenzi huo umefanywa na Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni ya China Bridge Engineering Group.

Amesema utekelezaji wa miradi hiyo ni mojawapo ya jitihada za Serikali za kuboresha miundomninu na kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment