Saturday, 9 April 2016

MAALIM SEIF KUTOA MSIMAMO WAKE URAIS WA DK SHEIN


Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad kesho ataelezea mwelekeo wake kisiasa, ikiwamo kufafanua kiundani uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20,2016.

Inadaiwa kuwa mkutano wa kiongozi huyo utakuwa wa kwanza  tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio na ataeleza mambo muhimu yatakayotoa picha halisi ya mwelekeo wake na CUF.

Uamuzi huo unafuatia ikiwa imepita takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la chama hicho kutoa msimamo wake wa kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na wawakilishi na madiwani.


Aidha, CUF  ilisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu baada ya Oktoba 28 mwaka jana kufuatia  Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya urais, uwakilishi na udiwani kwa madai  ya kuwepo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment