Monday, 25 April 2016

MAALIM SEIF AMGEUKIA KIKWETE


Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad amemtupia lawama Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akidai kuwa alitumia dola ‘kupindua’ demokrasia ili kuinusuru CCM iliyokuwa imeshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita kabla ya kufutwa.

Alisema Kikwete ambaye wakati huo alikuwa Amiri Jeshi Mkuu, anastahili lawama kwa kuwa alituma vyombo vya dola kugeuza uamuzi wa Wazanzibari waliokuwa wameufanya kupitia masanduku ya kura Oktoba 25 mwaka jana.’

Maalim Seif alisema hayo  wananchi walipomtaka kutoa neno la kuwasalimu alipopita katika Msikiti wa Ijumaa wa Masjid Swahaba, Mtoni Garagara, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Amesisitiza kuwa  watawala wanapaswa kutambua wananchi ndiyo huamua watu wanaowataka na siyo mabavu ya kulazimisha kwa kutumia dola au majeshi.

Mwanasiasa huyo aliwatoa hofu wananchi  na kusema kuwa  juhudi zinaendelea kuhakikisha haki ya uamuzi wao kupitia masanduku ya kura inapatikana.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha alifuta uchaguzi wa oktoba 25,2015 na kutangaza uchaguzi wa marudio Machi 20 mwaka huu ambao uligomewa na vyama 10 kati ya 14 vilivyoshiriki uchaguzi wa awali huku Dk Ali Mohamed Shein akishinda kwa asilimia 91.4.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment