Tuesday, 19 April 2016

Kashfa ya Rushwa Rais Dilma Roussef asema hatasalimu amriRais wa Brazil  Dilma Rousseff  amesema  hatasilimu  amri   baada  ya bunge  la  nchi  yake  kupiga kura  ili  kuanzisha  mashtaka ya  kumwondoa madarakani.
Akizungumza  kwa  mara  ya kwanza  tangu wabunge  wapige kura siku ya Jumapili, Rais Rousseff  amelalamika kuwa  ametendewa dhulma  kubwa huku akiongeza kuwa anazo nguvu, dhamira  na ujasiri, na kwamba ataendelea kupambana.
Zaidi  ya  theluthi  mbili ya wabunge  waliunga  mkono  hoja  ya kumfungulia mashtaka  kiongozi  huyo.

Baadaye Baraza  la seneti  litaamua  iwapo  atafunguliwa  mashtaka, mapema mwezi ujao au la ambapo. Wapinzani wa Rais Rousseff  wanadai  kwamba alichakachua mahesabu ya fedha  za serikali ili kujiongezea nafasi ya kuchaguliwa tena katika uchaguzi  uliofanyika  mwaka  2014 madai ambayo mwenye Bibi Rousseff ameyakanusha .

Reactions:

0 comments:

Post a Comment