Tuesday, 19 April 2016

Imekuwa Tofauti kwa Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar kurejea nchini humo


Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar aliyekuwa akisubiriwa kwa muda mrefu kurejea kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Juba, hajarejea kama ilivyotarajiwa mapema leo lakini msemaji wa Machar, William Ezekiel amesema wamejizatiti kwa ajili ya makubaliano ya amani, lakini kuna masuala ya kimipango na kiuongozi huyo badala yake kiongozi huyo atarejea Juba hapo kesho.
Kurejea kwa Machar na kuapishwa kuwa makamu wa kwanza wa rais, itakuwa ni hatua muhimu katika kuutekeleza mpango wa amani uliofikiwa Agosti mwaka 2015.
Makubaliano hayo yanaonekana kama matumaini mapya ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili na kuitumbukiza nchi hiyo changa katika mzozo  mkubwa wa kisiasa .

Reactions:

0 comments:

Post a Comment