Wednesday, 27 April 2016

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM YAUNDA KAMATI KUHAKIKI MALI ZAKE ZOTE


BARAZA la Madiwani la Jiji la Dar es Salaam limeunda kamati itakayohakiki mali zake zote zinazomilikiwa na jiji ili kuondokana na mbinu chafu zinazosababisha wananchi wasinufaike nazo.

Akiongea na wanahabari leo, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema kuwa kamati hiyo lazima ichambue mali hizo na zote zilizoko katika mikataba mbalimbali ili kujiridhisha kama taratibu zilifuatwa wakati mikataba hiyo ikiingiwa.

Amezitaja baadhi ya mali hizo kuwa ni pamoja na vibanda 130 vilivyo katika eneo la shule ya Benjamin Mkapa, Kariakoo ambapo waliopanga vibanda hivyo wanalipa Sh 30,000 kiwango ambacho ni kidogo ikilinganishwa na eneo vilipo.

Mwita amesema kuwa mali za jiji zimekuwa hazinufaishi jiji hilo na kufanya mapato yanayokusanywa kuwa Sh Bilioni 11.7 badala ya zaidi ya Sh Bilioni 20 iwapo makusanyo yake yatasimamiwa vizuri.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment