Friday, 1 April 2016

EWURA YASHUSHA BEI ZA UMEME NCHINI


Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushusha bei za umeme kuanzia leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti pamoja na kufuta kabiza tozo la huduma (service charge).

Kushuka huko kwa bei ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutaka bei za umeme zipunguzwe sambamba na hilo gharama za huduma kwa baadhi ya wateja zimeondolewa.

Bei mpya kwa watumiaji wadogo ni shilingi 100 kwa uniti moja, watumiaji wa kati ni shilingi 292 kwa uniti moja toka 298 ya zamani huku wafanyabiashara wadogo bei ikiwa shilingi 195 toka shiling 200 ya  hapo awali.

Bei mpya kwa wafanyabiashara wa kati ni shilingi 157 toka shilingi 159 na kwa wale wanaonunua umeme kwa wingi (bulk) ni shilingi 152 toka shiling 156 ya hapo awali.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment