Saturday, 9 April 2016

DK SHEIN AMPA UWAZIRI HAMAD RASHID


Rais  wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza la Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha uongozi wake wake kwa mujibu wa sheria huku mwanasiasa kutoka Chama cha Upinzani Hamad Rashid (ADC) naye akiingizwa katika baraza hilo.

Aizungumza wakati akitangaza baraza hilo Dr. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13, ambapo wizara tatu amezivunja na kuzigawa ndani ya hizo wizara 13 za sasa. Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7.

Ameongeza kuwa, mawaziri aliowatangaza leo atawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.

Baraza la Mawaziri la  Dr. Shein lina mawaziri   wafuatao;
1). Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Issa Haji Ussi Gavu.
2). Katiba na Sheria Utumishi wa Umma – Haroun Ali Sleiman.
3). Tawala za Mikoa na Idara maalum – Haji Omari Kheir.
4). Makamo wa 2 wa Rais – Mohamed Aboud.
5). Waziri wa Fedha na Mipango – Dk. Khalid Salum Mohamed.
6). Afya – Mahmoud Thabit Kombo.
7). Wizara ya Elimu – Riziki Pembe Juma.
8). Viwanda na Masoko – Amina Salum Ali.
9). Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Ali Karume.
10). Habari Utalii Utamaduni na Michezo – Rashid Ali Juma.
11). Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi – Hamad Rashid Mohamed.
12). Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mauldine Castiko.
13). Maji Ardhi Nishati na Mazingira – Salama Aboud Talib.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment