Monday, 4 April 2016

CUF KUTOA MSIMAMO KUHUSIANA NA MZOZO WA KISIASA ZANZIBAR


Chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar, Chama cha Wananchi (CUF), leo kinatarajia kutangaza mikakati na msimamo wake kuhusiana na mzozo wa kisiasa wa Zanzibar.

Msimamo huo unatarajiwa kuzungumzia muafaka kati ya chama cha CUF na CCM ambao ulileta uundwaji wa serikali kati ya vyama hivyo viwili.

Chama cha CUF visiwani Zanzibar hadi  sasa  bado  kinaendeleza  msimamo wake wa  kutotambua matokeo na serikali iliyoundwa kufuatia uchaguzi wa marudio uliompa ushindi Dk Ali Mohamed Shein.

Hivi karibuni shirika la misaada la Marekani MCC lilisitisha msaada  kwa madai ya kutoridhishwa na hali ya kisiasa visiwani Zanzibar.

Nchi  nyingine 10 kati ya 14 za mataifa ya ulaya nazo zimeungana na Marekani kusitisha msaada katika bajeti ya Tanzania kufuatia kuwepo mgogoro wa kisiasa Visiwani Zanzibar.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment