Wednesday, 27 April 2016

ACT WAZALENDO YAJAZA NAFASI YA KATIBU MKUU WAKE


Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha ACT-Wazalendo ilifanya kikao chake cha kawaida jana ( tarehe 25 Aprili 2016 Jijini Dar es Salaam.

Kufuatia kikao hicho chama hicho  kimemteua Ndugu Juma Saanani kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hadi pale uchaguzi mkuu wa ndani ya chama utakapofanyika.

Uteuzi huu unafuatia kung’atuka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Ndugu Samson Mwigamba anayekwenda masomoni katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Juma Saanani alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama (Zanzibar).

Reactions:

0 comments:

Post a Comment