Thursday, 10 March 2016

WENJE KUTUMIA MASHAHIDI 700 KUPINGA USHINDI WA MABULA, NYAMAGANA

wenje

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje anakusudia kuita mahakamani zaidi ya mashahidi 693 kupinga ushindi wa mbunge wa sasa, Stanslaus Mabula (CCM).

Wakili wa Wenje, Deya Outa aliieleza mahakama kuwa mashahidi hao ni pamoja na waliokuwa wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura, wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.

“Tunatarajia kuita mahakamani mashahidi wasiopungua 693 kuthibitisha madai yetu, kulingana na mahitaji ya hoja tunazotaka kuzithibitisha mahakamani,” alidai wakili Outa.

Kutokana na wingi wa mashahidi na muda wa mwaka mmoja uliowekwa kisheria wa mashauri ya uchaguzi kusikilizwa na kuamuliwa, wakili Outa alisema iwapo muda huo utaisha kabla hawajamaliza kutoa ushahidi wao, wataiomba mahakama kuwaongezea muda wa ziada.


Shauri hilo linalosikilizwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Kakusulo Sambo litaanza kusikilizwa Machi 14 mwaka huu

Reactions:

0 comments:

Post a Comment