Monday, 28 March 2016

SITA WAFARIKI USIKU WA PASAKA KATIKA AJALI YA BASI MJINI IRINGA


WATU sita  wamekufa  na   wengine  38 kujeruhiwa , baadhi yao vibaya, baada  ya  basi lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express Kutoka  Mwanza kuja  Iringa  kupinduka  katikati ya  Mteremko  wa Mlima Ipogolo  mjini Iringa wakati likielekea stendi ya Ipogolo,  kufaulisha  abiria  waliokuwa wakielekea mkoani  Mbeya.

Imeelezwa  kuwa baadhi ya  abiria  waliokufa  na  majeruhi   ni  wale ambao   walitakiwa kushuka stendi kuu ya mabasi yaendaye  mikoani ya mjini Iringa lakini hawakushwa kwa kile kilichoelezwa dereva wa basi hilo alikuwa akitaka kuwawahisha katika basi lingine lililokuwa likiwasubiri setndi ya Ipogolo abiria waliokuwa wanakwenda Mbeya.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Peter Kakamba alisema ajali hiyo ilitokea jana (juzi) saa 3:30 usiku baada ya basi hilo kumshinda dereva na kupinduka.

Kamanda alisema dereva wa basi hilo Castory Mwalusako (35) alikimbia mara baada ya ajali lakini polisi walifanikiwa kumkamata.

Mwalusako alisema basi hilo lilimshinda wakati akishuka mlima kutokana na kupoteza upepo kwenye brek, likapoteza mwelekeo na kupinduka.

Mganga mkuu wa mkoa wa Iringa Robert Salim alisema walipokea miili ya watu wanne waliofia katika ajali hiyo huku wengine wawili wakifariki baada ya kufikishwa hospitali hapo.

Dk Salim alisema waliokukufa ni wanaume wanne na wanawake wawili, maiti zilizotambuliwa ni mbili Makka Msigwa na Venant Mhagama aliyefia wodini.

Alisema majeruhi 38 walifikishwa hospitali ya Iringa ambapo 11 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 27 wamelazwa wachache wakiwa mahututi.

RPC Kakamba aliwataja waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo kuwa ni Banenda Helen (45) raia wa Kongo, Mbuyi Leoni (52) raia wa Kongo, Jojina Nyamboko (26) mkazi wa Songea,  Magambo Masunga (51) mkazi wa Mwanza,  Felister Mwinuka (19) mkazi wa Njombe, Tubilisiusy Selestine  (33), Said Kitonyi (17), Richard Bett (33) raia wa Kenya na Jofa Abonga (30)mkazi wa Geita.

Wengine ni Victor Lameck (25), mkazi wa Kagera, Pius Samwel (20) mkazi wa Mara, Michael Hadu (46) mkazi wa Madaba Songea, Hassan Mfaume (20) mkazi wa Iringa, Heriet Mwitinda (29) mkazi wa Arusha, Kiliana Kalinga (22) mkazi wa Mbeya, Hima Kifyasi (32) mkazi wa Bariadi, Omary Hassan (35) mkazi wa Makambako, Zuo Pawa (30) mkazi wa Mbeya, Chacha John (26) mkazi wa Iringa.

Wengine Timoth Sichoni (24) mkazi wa Dodoma, Ishimwe Jasmin (9) rais wa Rwanda, Mkagasana Sarafina (41) rais wa Rwanda, Zaina Kisaka (26) mkazi wa Manyara, Sara Sichone (26) mkazi wa Mwanza, Ivon Magaiwa (22)mkazi wa Mafinga, Solomoni Angolisye (58) mkazi wa Dodoma, Ivan Huwen (33) na mwingine ambaye hajajuliakana jina kutokana na kuwa na hali mbaya.


Mmoja wa shuhuda wa ajali hiyo James John alisema walitoka Mwanza vizuri na walipofika Iringa dereva alikataa kuwashusha abiria waliokuwa wakiishia Iringa ili awapeleke abiria waliokuwa wakienda mbeya kwenye basi nyingine eneo la Ipogolo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment