Wednesday, 9 March 2016

SERIKALI KUUNDA MAMLAKA KUU YA MAPATO YA TAIFA

TRAA

Serikali ipo kwenye mpango wa kuunda Mamlaka ya Mapato ya Taifa nje ya Mamlaka ya Mapato ya Taifa (TRA) iliyopo sasa ili kuondokana na malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.

Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Alphayo Kidata amewaambia wanahabari leo kuwa mamlaka hiyo itajumuisha taasisi zote zinazohusika na kukusanya mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko hasa yanayotokea katika halmashauri mbalimbali nchini.

“Mamlaka hii itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi wanazozifanya,” alisema.

Kidata amesema hatua hiyo ni mojawapo ya juhudi za serikali katika kuondoa kodi nyingi ambazo zimekuwa kero kwa wananchi wake.


Kamishna huyo ameongeza kuwa mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinazokusanya kodi watahakikisha wanalipatia ufumbuzi suala la kero ya kodi kwa wananchi bila kukandamiza upande wowote iwe serikali ama wananchi wa kawaida.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment