![]() |
WAKATI kukiwepo na taarifa za kuwepo kwa
dadapoa na kaka poa katika mikoa mbalimbali nchini ukiwemo mkoa wa Iringa, Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata dada poa pamoja
na kaka poa 287 katika operesheni maalum iliyofanyika maneo mbalimbali ya Jiji
hilo.
Oparesheni hiyo iliyoanza Machi 7, mwaka
huu baada ya kutangazwa kufanywa na Kamishna wa Kanda Maalum ya Jiji hilo,
Simon Siro aliyeazimia kuwakamata madada poa na makaka poa pamoja na wateja watakaobainika
wakiwanunua.
Katika mkoa wa kipolisi wa Ilala jumla ya
madada poa 51 kutoka katika maeneo mbalimbali yakiwemo msimbazi, Buguruni na
stakishari walikamatwa huku makaka poa 12 wakikamatwa katika maeneo ya Buguruni
na Msimbazi.
Huko Temeke jumla ya madada poa 22
walikamatwa, kati yao 12 walikutwa Chang’ombe na 10 Mbagala.
Katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, madada
poa 76 walikamatwa katika maeneo ya Osyterbay, Magomeni na Kawe ambako pia
makaka poa wanne walikamatwa.
CP Sirro amewataka watu wenye tabia kama
hizo kuacha mara moja kwani ni kinyume na mila na desturi za mtanzania na
akawataka watafute biashara nyingie halali za kufanya.
0 comments:
Post a Comment