Tuesday, 15 March 2016

NYUMBA YA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR YAPIGWA BOMU


Habari kutoka visiwani Zanzibar zinaeleza kwamba watu wasiojulikana wamerusha bomu na kulipua nyumba kadhaa ikiwemo ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame.

Habari hizo zinaeleza kwamba, Jeshi la Polisi linaendesha kamata kamata ya watu waliohusika kwenye tukio hilo ambapo mpaka sasa watu 31 tayari wametiwa mbaroni.

Tukio hilo limezidisha hali ya wasiwasi visiwani humo ambapo ni siku 5 tu zimesalia kabla ya uchaguzi  wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, mwezi huu.


Endelea kufuatilia mtandao huu kuhusu tukio hili kadri taarifa zaidi zitakapotufikia.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment