Wednesday, 23 March 2016

MWILI WA SARAH DUMBA WAAGWA NJOMBE MAPEMA LEO, KUZIKWA KESHO JIJINI DAR ES SALAAM


Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sara Dumba aliyefariki ghafla juzi jioni, amefanyiwa ibada leo mjini Njombe na kuagwa rasmi na wananchi wa wilaya hiyo na Mkoa wa Njombe kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam ambako mazishi yake yatafanyika.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Jackson Saikadau, amesema Dumba, anatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwake eneo la Mbutu Mwembe Mdogo Kigamboni na msiba wake utafanyika Kigamboni nyumbani kwa baba yake mzazi eneo la Ferry Midizini.

“Tunatarajia kuanza safari majira saa 10 jioni kutoka Njombe kwenda Dar es Salaam na maiti itawasili jijini humo alfajiri siku ya Alhamisi (kesho) kwa ajili ya taratibu za msiba na mazishi,”alisema.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment